July 28, 2018






MAISHA ya soka la ajabu sana. Yule Hassan Kessy ambaye alitua Yanga kwa mbwembwe akitokea Simba, msimu ujao hatavaa jezi ya Yanga.

Ndiyo hivyo tena wamemmwaga kwakile alichodai kwamba kuna figisu zilitokea wakati anadai chake ili asaini mkataba mpya. 

Kessy awali aliwaambia jamaa wampe Sh. milioni 60 lakini baadae akapunguza na kufikia Sh. milioni 45 na gari ambavyo. Yanga bado wakamwekea uso wa mbuzi.

Ishu imeenda kimasihara mpaka dakika za mwisho mara usajili ukafungwa. Lakini ametumia gazeti analoliamini la Championi Jumamosi kuwaambia mashabiki wa Yanga kilichotokea. Msikie.

“Kwa kifupi tu, nilishindwa kufikia muafaka mzuri na Yanga katika makubaliano yangu na wao, mimi nilikuwa nahitaji shilingi milioni 60 awali, lakini baadaye baada ya viongozi kuniambia hawana fedha hiyo, basi nikapunguza hadi 45 na gari la kutembelea.

“Nakumbuka nilimpa ofa hiyo alikuwa Tarimba (Abbas) baada ya kuniita ofisini kwake nikiwa na Yondani (Kelvin) kwa ajili ya kufanya mazungumzo hayo ambayo kwa upande hayakufikia mzuri.

“Nakumbuka baada ya mazungumzo hayo, Tarimba aliniambia nitakuita baada ya siku chache kwa ajili ya kumalizana naye, lakini cha ajabu ikawa kimya hadi usajili unafungwa.”

“Wakati usajili ukielekea ukingoni siku chache kabla ya kufungwa, niliwasiliana na bosi mmoja (jina tunalo) kuulizia hatma yangu kutokana na muda wa usajili kukaribia kufungwa na ndiyo nilipomuuliza akanijibu kwa meseji kwa kunitaka niwasiliane na Hussein Nyika (mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga) au Sanga (Clement, alikuwa kaimu mwenyekiti).

“Kwa maana hiyo, tayari kuna kitu kilikuwa kinaendelea kati yao viongozi juu yangu, kwa nini niongee naye (jina tunalo) halafu baadaye awatupie mpira akina Nyika na Sanga?

Mabosi wamfanyia umafia saa tisa kabla usajili kufungwa 
“Hakuna kitu nilichoumia na Yanga, licha ya wema wangu, kujitoa kwa moyo mmoja kuipambania timu bila ya kufanya mgomo wowote nikiwa na Yanga kama kupigiwa simu saa tisa mchana yakiwa yamebakiwa masaa machache kabla ya usajili kufungwa saa sita usiku na kuambiwa hatuna fedha za kukusajili tumeishiwa.

“Kauli hiyo ilitolewa na mmoja wa viongozi wa Yanga (jina lake amelificha) mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Yanga ambaye alimsajili Tshishimbi (Kabamba) kwa maana hiyo walikuwa wanataka mimi nikose timu ya kuichezea katika msimu ujao.

“Nashukuru nilishtukia hilo mapema nikajipanga nikijua litatokea hilo na kweli likatokea wao walitaka mimi nisaini kwa bei waliyokuwa wanaitaka wao shilingi milioni 30, hawakuwa na sababu yoyote ya kukaa kimya muda huo wote, wao wangeniambia tu mapema ningejua cha kufanya hata Mtibwa Sugar ningekwenda klabu yangu ya zamani.

Sasa unakwenda wapi?
“Sasa hivi nipo Zambia na nakaribia kufikia muafaka mzuri na moja ya klabu ya hapa nchini na kama mazungumzo yakienda vizuri nitasaini mkataba na baada ya kusaini tu haraka nitakutajia klabu yenyewe lakini kwa sasa siwezi kuitaja.”

Kipi ulichogundua kwa viongozi wa Yanga
“Wao wanashindwa kuthamini mchango wa wachezaji wazawa na hilo lipo wazi kabisa, kama mimi nimetoa mchango mkubwa ndani ya Yanga na katika kuthibitisha sijawahi kufanya mgomo wowote, licha ya baadhi ya wachezaji kugoma mara kadhaa kucheza kipindi ambacho hakuna mishahara, viongozi wa Yanga wao wanathamini wachezaji kutoka nje ya nchi. Ninaomba nilipwe mishahara yangu ya miezi mitatu ninayodai.

“Niwaambie Wanayanga kuwa, wawape ushirikiano wachezaji, benchi la ufundi na viongozi katika kipindi hichi kigumu ambacho Yanga inapitia ikiwa haipo vizuri kiuchumi.

“Ninaamini ipo siku Yanga watakaa vizuri na heshima ya timu itarejea, hivi sasa mimi ninahitaji tu mshahara wangu wa miezi mitatu ninayodai na ninashukuru nimeondoka kwa amani licha ya baadhi ya viongozi kunichafua hivi sasa kwa kuniponda kwenye mitandao baada ya kutosaini lakini wakati nikiwepo walikuwa wakinisifia,” anasema Kessy kwa huzuni mkubwa. 

Alipotafutwa Nyika ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa usajili kutaka kufahamu kuhusiana na ishu hiyo ya Kessy ambapo alisema kila kitu anakiweka wazi leo Jumamosi.

SOURCE: GAZETI LA CHAMPIONI.


7 COMMENTS:

  1. Huyu ni Kessy aliyeifungisha Simba kwa Yanga halafu kaondoka kwenda Yanga kwa mbwembwe zote? Ama kweli laana nyingine hapahapa duniani. Simba si alipewa gari na milioni 40 wakati wanamsajili. Zambia bora kwake atalipwa mara dufu kule.

    ReplyDelete
  2. Kabisa what goes around comes around. Kessy aliisaliti Simba kinyama kwa kuwazawadia yanga Goli. Kessy alikuwa kama beki wa Simba lakini aliamua kutoa pasi ya mwisho kwa Dornald Ngoma wa Yanga na kwenda kufunga. Kessy au wanaomuongoza ni wajinga wa tabia kwa hivyo wacha yawakute kwani ujuwaji uliopitiliza kiasi mara nyingi huzalisha ujinga.

    ReplyDelete
  3. Kessy hakuwahi kugoma? Kénya alikwenda kucheza na Gormahia? Analalamika wakati yupo Zambia angesajiliwaje dakika za mwisho wakati hayupo? Inashangaza.

    ReplyDelete
  4. Huyu mpaka maka jana akiisulubu simba kwa kila aina za kejeli lakini kun usemi " Kama hunijuwi, jaribu mwengine"

    ReplyDelete
  5. Aende Ndanda au Mbao, duuh kumbu usajili umefungwa? Ningekuwa yeye ningecheza hata bure ligi ya Rwanda. Kisha baadae arudi Yanga kama Ngasa alivyofanya kuwazimia simu simba wakati wanataka kumpa dili EL hilal ya Sudani. Hivi vyura fc huwa mnawapa nin wachezaji wa bongo hadi akili zinapotea kabisa?? Lakini Slamba alishituka

    ReplyDelete
  6. KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic