MKONGO WA YANGA AANIKA MBINU ZA KULIPIZA KISASI CHA BAO 4 ZA GOR MAHIA JUMAPILI HII
Kocha wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amefunguka kwa kuweka hadharani mbinu atakazozitumia kuwamaliza Gor Mahia FC.
Yanga na Gor Mahia zitakutana Julai 29 Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Zahera amesema dawa pekee ya kuwamaliza Gor Mahia ni kutumia madhaifu ambayo walionesha katika mchezo wa kwanza ambayo anaendelea kuyafanyia marekebisho hivi sasa.
Zahera ameeleza kwa sasa kikosi kipo kwenye ratiba ya mazoezi kuelekea mechi hiyo kubwa kwa Yanga hivyo wanajipanga kuhakikisha kuwa wanalipiza kisasi dhidi ya wababe hao wa Kenya.
Ikumbukwe Yanga ilikubali kichapo cha mabao 4-0 huko Nairobi na kujzidi kujiwekea mazingira magumu ya kusalia katika kundi hilo D ikiwa na alama moja pekee.








Anaota....
ReplyDeleteHaendi mtu uwanjani kwa kikosi kibovu hivyo
ReplyDeleteUsajili hovyo halafu mnataka watu waje kwenye mechi....hakuna kitu
ReplyDeleteKLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI UNAACHA WACHEZAJI KARIBIA 9, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA.....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA.....
ReplyDeleteKwa kweli kuna tatizo kubwa hapo Yanga!Hivi huyu Zahera Mwinyi ni kocha au rappa; mbona ana maneno mengi yasiyo na uhalisia? Kwanza ni kocha wa kujaa jukwaani akimwacha mchua misuli Mwandila aongoze kikosi. Tangu apewe kibarua Yanga imefungwa 4-0 mara mbili sasa, katika hali hii maneno yote haya ya nini, watuache angalau maumivu yaote sugu.
ReplyDelete