Unaweza kusema kwa kuwa alipumzika, basi atakuwa anahitaji muda wa kujiandaa sana.
Lakini mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi ameonekana kuwa fiti na anaendana na wenzake vizuri kabisa katika mazoezi ya kikosi hicho nchini Uturuki.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wako nchini Uturuki kuendelea kujiandaa na msimu mpya wa 2018/19.
Okwi aliruhusiwa kupumzika kutokana na kuwa majeruhi, hivyo hakushiriki michuano ya SportPesa Super Cup pamoja na ile ya ambayo yote Simba ilifika fainali lakini haikubeba ubingwa.
Okwi ameonekana kuwa vizuri akishirikiana na wenzake vizuri kwa kiwango kizuri kabisa.
Ratiba ya Kocha Patrick Aussems raia wa Ubeligiji inaonyesha Simba itaendelea kupasha leo huku akiendelea kuongeza aina tofauti ya mazoezi.







Kaka Okwi ni professional. Kwani ushaliwahi kumuona Daktari kaenda likizo alafu aliporudi kazini akaelekezwa jinsi ya kumdunga mtu sindano? Ukimwangia Okwi ni mchezaji mwenye mwili mwembamba lakini uliojengeka sio goigoi inaonekana ni mtu makini hata katika matunzaji ya mwili wake na huo ndio uprofessional.
ReplyDelete