Kufuatia kifo cha Mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric James Shigongo, marehemu Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia leo Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu, Meneja Mkuu wa Global Publishers ametoa ratiba ya kuaga na mazishi ya mpendwa wetu huyo.
Akizungumza na Global TV Online, Mrisho amesema mwili wa marehemu utatolewa katika chumba cha kuhifaadhia maiti kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kesho Jumamosi na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B, jijini Dar es Salaam ambapo utalala hapo.
Jumapili saa 3:00 asuhuhi shughuli ya kuaga mwili itaanza na baadaye utapelekwa kanisani kwa ajili ya ibada maalum na maombi kisha utasafirishwa kupelekwa jijini Mwanza kwa ajili ya mazishi ambapo utaagwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Nyakato Mecco, Mwanza Mjini Jumatatu kisha kusafirishwa tena kwenda katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa wilayani Sengerema, kwa ajili ya mazishi.
Bi. Asteria Kapela atapumzishwa katika nyumba yake ya milele, nyumbani kwake Bupandwamhela Jumatano ijayo ya Agosti 1, 2018 ambako ndiko alikozikwa mumewe, marehemu Mzee James bukumbi.
0 COMMENTS:
Post a Comment