July 25, 2018


Na George Mganga

Wachezaji wawili wa klabu ya Yanga, Mateo Anthony na Deus Kaseke usajili wao umekamilika katika Shirikisho la Soka Africa (CAF).

Usajili wa awali wa Anthony ulishindwa kupitishwa na CAF kutokana na kuwa na makosa kadhaa ambayo yalisababishwa na utofauti wa majina yake yaliyotumwa lakini sasa umefanyiwa marekebisho.

Mbali na Anthony, kiungo mshambuliaji, Kaseka aliyerejea Yanga baada ya kuichezea Singida United kwa msimu uliopita 2017/18 usajili wake umepitishwa moja kwa moja na sasa wachezaji wote wamepata leseni ya kushiriki mashindano ya CAF.

Kaseke na Anthony sasa wapo huru kukipiga dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Julai 29 watakuwa wancheza dhidi ya Gor Mahia FC.

Wakati wachezaji hao wawili wakipata leseni hizo. kikosi cha Yanga kinaendelea na programu za mazoezi kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Gor Mahia chini ya Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic