BEKI SIMBA AMTUPIA SIFA KEDEKEDE CANNAVARO
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya mchezo la Soka la Ufukweni ‘Beach Soccer’ Boniface Pawasa amefunguka kuwa kitendo cha uongozi wa Yanga kumpa jukumu la umeneja wa timu hiyo, beki wake Nadir Haroub Cannavaro ni cha kupongezwa.
Pawasa amesema kuwa Cannavaro amestahili kupewa nafasi hiyo kutokana na nidhamu, uzalendo na kujituma kuitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu bila kuwa na migogoro kama baadhi ya wachezaji wengine.
Pawasa ambaye aliwahi kuichezea klabu ya Simba nafasi ya beki, ameeleza kuwa Cannavaro amekuwa na uzalendo mkubwa Yanga ukiachilia na wachezaji wengine ambao wamekuwa sehemu ya timu hiyo.
“Amekuwa kiongozi bora ndani na nje ya uwanja huku akitoa mchango mkubwa kwenye timu ya taifa lakini pia amekuwa tofauti na wachezaji wengi wakongwe waliopita klabuni hapo kwa kuonyesha uzalendo na kusisitiza nidhamu na uvumilivu kwa wachezaji pindi inapotokea sitomfahamu.
“Kwanza nimpongeze mdogo wangu Cannavaro kwa hatua aliyofikia kwani ni matunda aliyoyavuna kutokana na mbegu bora ya nidhamu aliyoipanda, Cannavaro ni mtu aliyezaliwa kuwa kiongozi kila mtu aliona jinsi alivyoitumikia Yanga kipindi anacheza hivyo naamini atafi ka mbali sana hususani kwenye tasnia hii ya soka,” alisema Pawasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment