April 25, 2019


KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa yeye ndiye alimtimua meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kuonekana kwenye ofisi ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji Mo licha ya yeye kufafanua kuwa alikuwa na ishu zake.

Lakini siyo hilo tu, Zahera amemhusisha staa huyo wa Zanzibar mwenye heshima Yanga na bao walilofungwa na Meddie Kagere kwenye mechi ya mwisho ya watani.

Cannavaro ambaye baada ya kustaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita alikabidhiwa cheo hicho, ametimuliwa na kocha huyo kwa madai kuwa anawasaliti na amekuwa na washikaji wengi sana wa Simba katika miezi ya hivi karibuni.

Zahera ameliambia Championi Jumatano kuwa, amefikia uamuzi wa kumtimua baada ya kufuatilia matendo yake kwa muda mrefu, lakini kubwa ni hilo la kuonekana kwenye ofisi ya bosi huyo wa Simba wakati Yanga ikiwa kwenye mapambano.

Mbali na sababu hiyo, pia Zahera anadai Cannavaro aliihujumu Yanga kabla ya kucheza na Simba Februari, mwaka huu na kufungwa bao 1-0 ambapo akiwa kama meneja, aliwaruhusu wachezaji kutoka usiku bila ya kocha kufahamu kitu chochote.

“Cannavaro hayupo kwa sababu alionekana katika ofisi ya bosi wa Simba anaingizwa mlango wa nyuma, watu walimuona, wakapigiwa simu viongozi wa Yanga kuambiwa kuwa Cannavaro, ameonekana akiingia katika ofisi ya bosi wa Simba, jioni alipoulizwa alisema kuwa alienda kumtafutia mke wake kazi.

“Lakini hili ni tukio la mara ya pili tulikua Morogoro kujiandaa na mechi ya Simba na siku mbili kabla ya mechi aliwaruhusu wachezaji watatu saa mbili na nusu usiku kwenda kukimbia mbio nje ya hoteli, waende hadi mjini bila ruhusa yangu.

Zahera aliongeza kuwa: “Kesho yake yule mtu wa ulinzi akaniambia kwamba Cannavaro aliruhusu wachezaji watatu kutoka usiku waenda kukimbia mbio, nikamuuliza walitoka dakika ngapi, mlinzi alisema hawakuchukua hata dakika 15 wakarudi.”

“Sasa siunaona kuna tatizo hapo nadhani siwezi kukubali mtu kama huyo katika benchi langu kutokana na mambo hayo,” alisema Zahera.

Hata hivyo, alipotafutwa Cannavaro simu yake haikupatikana huku ikidaiwa kuwa amekuwa akitumia simu ya ndugu yake kwa ajili ya kuwasiliana na watu wake wa karibu na hakuna ambaye tupo tayari kutoa namba hiyo. 

Cannavaro ni mmoja kati ya wachezaji wa zamani wa Yanga ambapo alicheza kwa zaidi ya miaka kumi akiwa ametwaa makombe kadhaa makubwa.

CHANZO: CHAMPIONI

9 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Uongo mtupu....Hakuna habari kama hiyo, waandishi wetu na vyombo vingi vya habari vimekuwa vikizusha habari za uchochezi, ili kuivuruga Yanga. Hizi ni mbinu za maadui kutaka kuidhoofisha Yanga....mara nyingine nasema hazitafanikiwa!

    ReplyDelete
  3. Inawezekana uongo na naomba ibaki kuwa uongo, lakini kama ni kweli bado sioni Cannavaro huyu leo hii abadilike hivyo, siamini. Na kwanini awe na mahusiano mabaya na kocha tuangalie pande zote mvili kwasababu jamani Cannavaro tumetoka nae mbali. Kweli ni wa kuachana nae ?Hata ingekuwa kwenda
    kwa Mo hawezi kuurza timu yake aliyoitumikia kwa mapenzi sana zaaide ya neus ya umri wake inawezekana kweli anamtafutia kazi mkewe hivi alitakiwa amuombe kocha ruhusa? cannavaro ni kiongozi na mtu anayejitambua sanasana ushauri wangu tusimtoe kafara bado tunamuhitaji. Kocha aelezwe wakati huu tunamuhitaji sana cannavaro tusimpoteze.

    ReplyDelete
  4. Huyu Zahera ni mtu mwenye vituko vya aina yake, yaani anaamini Simba sio ya kuifunga yanga aliyokwisha kuivuruga. Amekuwa akiwavaa vibaya wenye heshima zao na mmojawao huyu Canavaro ambaye ameifanyia yanga makubwa sana na leo tunashuhudia akimsingizia mengi na kumfukuza kama mbwa koko. Huyu kaja kuibomowa yanga na wala sio kuijenga na mwingi wa majisifu na kujiona mwenye jina kubwa kwenye ulimwengu wa Soca.

    ReplyDelete
  5. Zahera Awe Makini Atawaharibu Kisaikolojia Wachezaji Wa Yanga Maana Kila Kitu Kibaya Hajihusishi Kama Yeye Ndo Chanzo Sasa Ona Alivyo Msingizia Cannavaro Mbona Yanga Walisitahili Kupigwa Goli Nyingi Tu Vipi Michezo Mingine Aliyo Poteza Je Ni Cannavaro Kahusika Na Wajiande Kipigo Kutoka Kwa Azam Fc

    ReplyDelete
  6. Huyu Kocha ni kama masikio yaliyozidi kichwa.
    Hana wa kumsemesha, anafanya atakayo kama anaendesha shamba la urithi.

    ReplyDelete
  7. Na yanga wanajivunia naye wanaona wamepata mtu hapana timu iliyowahi kupata, anamtaka anayemtaka, anatamka anayotaka na anamfukuza anayemtaka kwa huria yake

    ReplyDelete
  8. Ukiwa fukara huwezi chagua. Beggars cannot choose.Huwezi kuwa huru.

    ReplyDelete
  9. huyu Zahera hajiulizi kama kweli kafanya hivyo kwa cannavaro kama kocha lakini cannavaro ni meneja wa timu na zahera kamkuta cannavaro akiwa yanga au anataka hyo nafasi akaimu yeye maana sasa hatumuelewi ila kwa kuwa hakuna aliyejuu yake ngoja sasa aibomoe timu lakini akumbuke yeye ni mwajiriwa tu sasa anataka kufanya mambo bila hata kujali wadhifa alionao yanga. Nilimsikia anasema hata hizi faini anaweza kulipa lakini hawatakubali kuingilia mlangoni mwa geti lililopangwa sasa anajenga au anabomoa timu ya yanga akumbuke wangapi wamepita yanga na wakaipa mafanikio ya timu ya yanga. SO afanye yake na sio hayo anayoyafanya. Yanga bila simba si yanga imara na Simba bila yanga si simba imara. kaeni vizuri watani wangu tupige mzigo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic