Wakongwe
wa DR Congo, Vita Club imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya
kushinda kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia.
Maana
yake Wakongo hao wamefuzu kwa jumla ya mabao 4-2 kutokana na ushindi wa 2-1
katika mechi ya kwanza mjini Kinshasa na sasa wanawasubiri TP Mazembe.
TP
Mazembe inacheza leo dhidi ya Entente Setif ya Algeria.
Mazembe
inayoongozwa na Mbwana Samatta kwenye safu ya ushambuliaji itakuwa nyumba
Lubumbashi.
Vita
walikuwa mabingwa wa kombe hilo mwaka 1973 lakini mwaka 1981, wakafanikiwa
kuingia fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment