August 11, 2018


Kuelekea mechi maalum ya kumuaga aliyekuwa beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro, uongozi wa klabu hiyo umesema utaistafisha jezi yake.

Cannavaro aliyekuwa akivaa jezi namba 23, jezi hiyo itapigwa STOP na haitoweza kutumika tena kutokana na kumuwekea heshima mchezaji huyo ambaye amepewa wadhiwa wa Umeneja wa Timu kwa sasa.

Kitendo hicho kitafanyika Agosti 12 ambapo Yanga itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market mjini Morogoro utakaokuwa wa kumuaga Cannavaro.

Yanga imeweka kambi mjini Morogoro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu pamoja na maandalizi ya kukipiga na USM Alger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Agsosti 19 mwaka huu jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic