STRAIKA HATARI KOTOKO ALIYEWAPA TABU WAWA NA NYONI TAIFA KUTUA SIMBA
Simba hii acha kabisa, ni kama utani vile lakini taarifa ikufikie tu kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuvutiwa zaidi na rasta wa Asante Kotoko, Yacouba Songne, imeelezwa.
Aussems ameeleza kuwa straika huyo ni balaa tupu na akisema kama isingekuwa dirisha dogo basi angefanya mazungumzo na mabosi wake ili kumsajili straika huyo hatari.
Mapema mara baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Kotoko kumalizika pale Uwanja wa Taifa, Agosti 8, Mbelgiji huyo alifunguka na kueleza hakuna Kocha ambaye anaweza akaacha kumsajili mchezaji wa aina kama ile.
Katika mechi hiyo, Songne aliupiga mwingi mno na kuwapa tabu zaidi mabeki wa Simba ikiwemo Pascal Wawa na Erasto Nyoni.
Hata hivyo amesema ayafanya mchakato wa kuzungumza na waajiri wake ikiwezekana katika dirisha dogo aweze kusajiliwa na timu hiyo ambayo kwa sasa ina jeuri na fedha za mwekezaji wake, Mohammed Dewji Mo.
Wakati Mbelgiji huyo akifunguka juu ya Songne, Simba ipo mjini Ruangwa hivi sasa na leo inashuka dimbani kukipiga na Namungo FC kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa.
Simba kila mchezaji mnamtaka tengenezeni timu ya pili nayo. Kwenye ligi ya mabingwa kila timu mtakayocheza nayo mkiona mchezaji mzuri tu mtakuwa mnataka kumsajili.
ReplyDelete