August 10, 2018


Kocha wa Dodoma FC na Mwanachama wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola juu ya tamko lake la kupambana na wauza jezi feki.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Lugola kusema atakula sahani moja na wauza jezi wote feki ambao wamekuwa wakizitengeza na kusababisha mapato ya klabu kupotea kihuni.

Kauli ya Waziri huyo aliyeanza kazi kwa kasi kubwa, imefanya Julio kutoa pongezi zake kwa Lugola na akiomba juhudi ziwe kubwa ili kuwabana wapigaji hao wa mjini.

Julio amesema baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitengeneza jezi hizo wanapaswa kuwajibishwa kutokana na kuinyima klabu faida na akiamini kuwa sasa watapata wakati mgumu kutokana na Waziri Lugola kuingilia kati.

Aidha, Kihwelo amewataka pia Simba kuongeza nguvu za kupambana nao kwa kushirikiana na Waziri Lugola juu ya uuzaji wa jezi ili kuepuka matapeli ambao wamekuwa wakitengeneza jezi bandia na kuuza mtaani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic