August 10, 2018


Staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid amefanikiwa kumshawishi rapa mkongwe kutoka Marekani, P Diddy kwenda nchini Nigeria.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wizkid anayebamba na Albamu ya Sounds From The Other Side aliweka kipande cha video kikimuonesha akiwa na P Diddy pande za New York akisisitiza kwenda nchini Nigeria.

“Naweka sawa, naweka sawa, najua mnajua kuwa nakuja kwenye ardhi ya nyumbani,” alisikika P Diddy. Naye Wizkid aliyekuwa amevalia ‘traksuti’ yenye chapa ya Dolce & Gabbana alisema; “Nitakukumbuka sana!”  Mara ya mwisho kwa P Diddy kufika nchini humo ilikuwa Julai, 2014.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic