August 10, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umelaani vikali tukio la Polisi kumpiga Mwandishi wa Habari za Michezo Sillas Mbise ambeya alikuwa akikusanya habari katika tamasha la Simba Day Agosti 8 Jumatano ya wiki hii.

Kupitia Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah 'Try Again' amesema tukio hilo halifuahishi kutokana na mchango wa Wanahabari kwa ujumla juu ya mchango ambao wanatoa.

Again ametoa pole zake za dhati kwa Wanahabari wote kwa ujumla juu ya Mwandishi huyo aliyepigwa na askari hao wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alipokuwa ndani ya Uwanja kuzungumza machache kabla ya pambano kuanza.

Kitendo cha Mbisse kupigwa kilisababisha Waziri Lugola kuingia na ndipo ikafikia hatua ya Mwandishi huyo kutolewa nje ya Uwanja kwa usalama zaidi.

2 COMMENTS:

  1. PT Piga Tu!! Wakishamaliza kupiga kisha wanaomba ushirikiano na raia!!!
    Aisee hatari sana haya mambo ya urafiki wa mashaka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Raia wa Tanzania wakiongozwa na waandishi wa habari wengi ni maboya..
      Kupigwa wanapigwa; kulalama wanalalama..
      Ila wakiomba ushirikiano wanatoa bila kinyongo..!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic