KIONGOZI SPUTANZA AWACHANA STAND UNITED JUU YA USUGU WA KUTOLIPA MISHAHARA YA WACHEZAJI
Mwenyekiti wa Chama kinachotetea na kulinda haki za wachezaji nchini (SPUTANZA), Mussa Kisoki, amewachana Stand United kutokana na tabia ya kutolipa mishahara ya wachezaji wao.
Kisoki amefunguka na kueleza kuwa Stand imekuwa timu ya ajabu kuwahi kutokea kutokana na malalamiko ambayo baadhi ya wachezaji wake wamekuwa wakiyatuma kwenye chama hicho.
Kiongozi huyo amesema imekuwa ni kawaida kwa wachezaji wa klabu hiyo kutolipwa mshahara wa miezi miwili mpaka mitatu, kitu ambacho kinapelekea kuvunja mikataba yao.
Ikumbukwe kabla ya dirisha la usajili kuelekea ukingoni, beki aliyekuwa anaichezea Stand, Ally Ally aliibuka na kusema hajalipwa mshahara wa miezi mitatu na kuamua kuvunja mkataba wake na baadaye akatangazwa kusajiliwa na KMC FC iliyopanda daraja kushiriki Ligi Kuu msimu wa 2018/19.
Aisha, Kisoki amewataka Stand kama hawawezi kufanya shughuli za mpira ni vema wakafanya shughuli zingine au wawaachie watu wengine ambao wanaweza kuiendesha klabu hiyo.
Mimi wasia wangu ni kuwa timu zisizokuwa na uwzeo wa kuwalipa mishahara yao wachezaji wakinaike na uwezo waliokuwa nao na kamwe wasijaribu kumuiga tembo kumeza boga na wakaadhirika mbele ya safari na kupambana na migomo ya usiku na mchana
ReplyDeleteMusa Kisoki amesema vizuri sana. Huna uwezo wa kulipa mishahara wachezaji na makocha wa time FUNGA duka. Tafuta biashara nyingine ya kufanya hii ya mpira huiwezi. Mnafanya dhambi kubwa kuwatesa wachezaji kwa kutowalipa mishahara yao ambayo ni haki yao. Tabia sio nzuri.
ReplyDelete