August 11, 2018


Wakati kikosi cha Yanga kikijiandaa na mchezo maalum wa kumuaga beki wake mkongwe, Nadir Haroub 'Cannavaro', dhidi ya Mawenzi Market, uongozi wa klabu hiyo umesema mshambuliaji wake, Matheo Anthony hajawa fiti.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika, amesema Athony bado hajapona vizuri baada ya kuumia mazoezini wakati kikosi kikiwa mjini humo.

Nyika ameeleza kuwa mshambuliaji huyo aliumia mkono japo matumaini ya kucheza dhidi ya Mawenzi Agosti 12 yapo.

Yanga imekita kambi ya wiki mbili mjini Morogoro kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Agosti 19 mwaka huu.

Nyika amesema ambi hiyo ya Morogoro imeonesha matumaini kutokana na juhudi za wachezaji namna wanavyojituma Uwanjani na wakipokea mafunzo kutoka kwa Kocha wao, Mwinyi Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic