August 10, 2018


Mwanachama wa klabu ya Yanga anayejulikana kwa jina la John Njembele ameibuka na kuungana na Katibu wa Baraza la Wazee Yanga akiitaka Yanga ifanye uchaguzi mpya ili kumaliza matatizo yaliyopo.

Njembele ameeleza kuwa ili Yanga iweze kurejesha makali yake amewataka viongozi wa Kamati ya Utendaji waliosalia wajiuzulu ili uchaguzi mpya ufanyike.

Mwanachama huyo amesikika kupitia radio moja hapa nchini akieleza kuwa viongozi hao wote waliopo kwenye Kamati ya Utendaji wamekuwa wakisababisha mambo ndani ya klabu yashindwe kwenda sawia.

Siku kadhaa zilizopita, Katibu wa Baraza la Wazee, Mzee Akilimali naye aliibuka na kusema ili Yanga iweze kumaliza mpito ambao klabu inapitia kwa sasa ni vema ikafanya uchaguzi haraka.

Ikumbukwe hivi karibuni, baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo walitangaza kujiondoa Yanga kutokana na kukosa maelewano mazuri kati yao na uongozi wa juu ikiwemo Salum Mkemi na Khalfan Hamis.

3 COMMENTS:

  1. Je kipindi cha mpito hao kina Ailitele na genge lake wameisaidiaje klabu? Je huo uongozi mpya unaotarajiwa utakuwa na miujiza mipya ya mapato ili kutatua matatizo ya kiuchumi na ukosefu wa mishahara ya wachezaji? Je walipopinga Yanga Kampuni na Yanga Yetu hawakujua nini matokeo? Wanachama mfu wenye mawazo na fikra mfu hawataivusha nchi kimichezo wala kuuza klabu kwa maana wanawaza upigaji na unazi

    ReplyDelete
  2. Soka l bongo magumash 2 ftina nying soka Hanna k2 km tm angpew manj kw miaka 10 umaskn huu w fedha ucngekuwepo.

    ReplyDelete
  3. Soka l bongo magumash 2 ftina nying soka Hanna k2 km tm angpew manj kw miaka 10 umaskn huu w fedha ucngekuwepo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic