August 10, 2018


Na George Mganga

Baada ya kushindwa kutangazwa katika orodha ya wachezaji ambao walihusika na tamasha kubwa la Simba Day Agosti 8, uongozi wa klabu hiyo umefunguka juu ya Haruna Niyonzima na Juuko Murushid.

Kwa mujibu wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah maarufu kama Try Again, amesema kukosekana kwa wachezaji kutambulishwa katika tamasha hilo haina maana kuwa wameachana nao.

Akizungumza kupitia Radio Magic FM, Again ameeleza kuwa Juuko na Niyonzima watakuwa nao siku za usoni kwasababu bado ni mali ya klabu huku wakiwa na mikataba.

Aidha, Again amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuipenda klabu na kuondoa hofu kwa wachezaji akiwa anaamini bado kina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri hata wasipokuwepo.

"Kuhusu suala la Haruna Niyonzima na Juuko Murushid kutotangazwa Simba DAY jana, halimaanishi kuwa si wachezaji wetu, wachezaji hao watakuwa nasi siku za usoni kwa maana bado ni mali yetu. Kingine wapenzi na wanachama wa Simba wananapaswa kuipenda klabu na si kuonesha hofu kwa wachezaji" alisema.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic