September 8, 2018


Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, arejee nchini kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu, afya ya kiongozi huyo inaripotiwa imeanza kuimarika kwa sasa.

Mkwasa ambaye alijiuzulu kuwa katibu wa Yanga hivi karibuni baada ya hali yake ya afya kuwa mbaya na kusababisha apelekwe India ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo, hali yake inaendelea vizuri.

Mke wa Mkwasa, Betty Mkwasa alisema hali ya Mkwasa inaendelea vizuri na sasa ameshaanza kufanya mazoezi ya kutembea mwenyewe lakini pia madaktari wa India wamekuwa wakiwapa msaada wa kimati­babu kutoka nchini humo.

“Hali yake inaendelea vizuri sana kwani ame­shaanza mazoezi ya kutembea mwenyewe lakini pia madaktari wa India kila siku tunaongea nao juu ya hali yake, kuhusu ku­rudi kwenye majukumu yake ni mpaka miezi mitatu ipite ndiyo madaktari watam­ruhusu ni kazi gani ambayo anatakiwa kufanya,” alisema Betty.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic