MBELGIJI AMWEKEA MTEGO STRAIKA SIMBA
Kocha Mkuu Simba Mbelgiji, Patrick Aussems ametaja sababu ya kuagiza mchezo wa kirafiki katikati ya Ligi Kuu Bara kuwa ni maalum kwa ajili ya wale wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi chake cha kwanza.
Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki kesho Jumamosi saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya FC Leopards ya nchini Kenya.
Baadhi ya wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi chake ni kiungo,
Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Marcel Kaheza, Adam Salamba na Mohamed Rashidi.
Aussems alisema mechi hiyo maalum kwa ajili ya wachezaji hao na kikubwa anataka kuwaona zaidi wakiwa uwanjani wakicheza mechi badala ya mazoezi pekee.
Aussems alisema, mechi hiyo itawasaidia wachezaji hao kujenga hali ya kujiamini kama siku moja ikitokea mmoja wapo akapata nafasi ya kucheza, basi acheze kwa kiwango kikubwa.
“Katika usajili wangu wa msimu huu, nina wachezaji 27 ambao wamesajiliwa wote wana uwezo mkubwa wa kucheza katika kikosi cha kwanza lakini tatizo ni nafasi pekee.
“Hivyo, nimeomba mechi hii ya kirafiki na Leopards makusudi kwa lengo la kupata nafasi ya kuwaona wachezaji wangu wakiwa uwanjani wakicheza na hii itawasaidia wachezaji kuongeza hali ya kujiamini uwanjani.
“Siku zote mchezaji akifanya mazoezi muda mrefu katika timu bila ya kucheza ni ngumu kutathimini kiwango chake na hata yeye mwenyewe hali ya kujiamini itaondoka, hiyo ndiyo sababu ya kuagiza mechi hiyo,” alisema Aussems.








0 COMMENTS:
Post a Comment