September 30, 2018


Kuelekea mechi ya watani wa jadi leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mchezaji wa zamani wa Yanga amesema timu yake ina nafasi ya kushinda kwakuwa inaingia mchezoni bila presha.

Chambua ameeleza kuwa Yanga inaenda kucheza na Simba ikiwa haijapoteza mchezo wowote katika minne iliyopita pia ikiwa haijaenda suluhu ama sare.

Mchezaji huyo aliyewahi kutamba na Yanga miaka ya nyuma, anaamini Yanga inaweza ikapata matokeo dhidi ya Simba ambao wanakuja uwanjani kusaka matokeo kibabe kutokana na kwenda sare mchezo mmoja na kupoteza dhidi ya Mbao.

Aidha, Chambua amesema kutokupoteza ama kwenda suluhu kwa Yanga hakuna maana kuwa itapata matokeo kirahisi bali ni kwa kupambana na kutumia vema nafasi ambazo wanazitengeneza uwanjani.

Kupatikana kwa matokeo Chambua anaamini itategemea na nidhamu ya mchezo wa Yanga akieleza kuwa Simba wana kikosi kipana na wao hawaendi kucheza bali ni kusaka ushindi pekee.

"Yanga wanaweza kushinda mechi ya leo lakini wanapaswa kupambana haswa kwa maana Simba ina kikosi kipana ambacho kinaingia dimbani kusaka alama tatu kama wao pia" alisema.


3 COMMENTS:

  1. Chambua Acha Mchecheto kipigo kipo Palepale kwa Simba

    ReplyDelete
  2. Chambua acha maneno...subir game uwanjan..cha moto kinawahusu..

    ReplyDelete
  3. Chambua simba haina presha ndiyo maana haikulimbia jiji kwa maandalizi ya mechi hii , jiandaeni kisaikrojia kupokea kipigo cha mnyama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic