September 20, 2018


Na George Mganga

Kwa mara ya kwanza klabu ya Mbao imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara umemalizika kwa bao pekee kufungwa na Said Hamis mnamo dakika ya 26 kwa njia ya penati baada ya kipa Aishi Manula kumdondosha straika wa Mbao, Pastory Athanas kwenye eneo la hatari.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kusalia na alama zake 7 huku Mbao ikifika kileleni kwa kujikusanyia pointi 10.

Aidha, mechi nyingine mbili za Ligi Kuu Bara zilipigwa leo ambapo Kagera Sugar ikiwa ugenini Mbeya imelazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tanzania Prisons.

Singida United waliokuwa Uwanja wa Uhuru kucheza na African Lyon wamepokea kichapo cha mabao 3-2.

7 COMMENTS:

  1. hiyo ndiyofaida ya kucheza mpira mdomoni

    ReplyDelete
  2. Wapigwe tuu hatuna habari, mpaka wachezaji wa kikosi cha pili walioachwa dar watakapoiva.. mnamuacha kocha aliyeifanya timu itishe last season nyumbani..tunamuacha kocha ambaye ameirudisha timu nyuma mara 10 ndio anafundisha na timu inacheza hovyo licha ya kuwa na nyota kibao.. Simba tukapimwe akili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na watapigwa sana..Mtwara walicheza hovyo.Simba sio timu ya kufungwa goli moja na wakashindwa rudisha...Angekuwa Djuma halo Simba wangepiga mbili

      Delete
  3. Hata George hapo unaonyesha dhahiri wewe ni timu gani.Hivi Uturuki wanacheza Mpira tofauti na kwingineko duniani.Lazima ujue kuna vitu standard....mwanafunzi wa chuo kikuu Uturuki ni sasa na wa chuo kikuu Morogoro..mazoezi wanayofanya ni standard...na wanacheza mpira unaofuta kanuni zile zile.na mazoezi ni yale Yale...Mganga acha upuuzi

    ReplyDelete
  4. haooooooo! wazee wa uturuki na safar hii tutakutana wakati tumewazd point kochokocho,mutainamsha sana vchwa kwa aibu mwaka huu sisi tunapeta tu na michango yetu,chezea jangwani wewe wazee wa 4G.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic