September 8, 2018



Kikosi cha Taifa Stars, kimelazimishwa sare ya bila kufungana kikiwa ugenini dhidi ya wenyeji wake Uganda.

Mechi hiyo ya kuwania kufuzu Afcon imepigwa kwenye Uwanja wa Namboole jijini Kampala na Stars iliyokuwa ikiongozwa na nahodha Mbwana Samatta imeonyesha soka safi na kuwapa wakati mgumu Uganda.

Stars ilifanya mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Uganda, hasa katika kipindi cha pili, hali iliyowalazimisha walinzi wa Uganda kufanya faulo nyingi zaidi.

Kipindi cha kwanza ilionekana Uganda wakiwa na nafasi nyingi ambazo hawakuzitumia huku mvua kubwa iliyonyesha dakika chache kabla ya mechi ikiwa imechangia kuvurugika kwa uwanja huo.


Hata hivyo, kipindi cha pili, Waganda walishambulia kiasi huku Stars kupitia Samatta, Thomas Ulimwengu na Saimon Msuva wakionyesha kiwango cha juu. Nafasi kadhaa nao walishindwa kuzitumia.

Mabeki kam Abdi Banda, Aggrey Morris, Hassan Kessy, David Mwantika, Gadiel Michael wakishirikiana na viungo Frank Domayo, Mudathir Yahaya na Himid Mao aliyeingia baadaye wakioneysha soka la kiwango cha juu.

Stars inayonolewa na Kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike, imefikisha pointi 2 katika Kundi L linaloongozwa na Waganda wenye pointi.





11 COMMENTS:

  1. Taifa Stars imelazimisha sare Uganda nadhani hicho ndicho kingekuwa kichwa sahihi cha habari kwa maoni yangu. Kulazimisha sare na Uganda nyumbani kwake sio jambo dogo hongereni vijana ila ukweli lazima tuuseme na asiependa au kutokubaliana ni uamuzi wa mtu Tanzania ni nchi huru mtu kutoa mawazo yake hata kama yanakera. Kiukweli ni kwamba mkanganyiko uliotokea wa kuondolewa kwa wachezaji wa Simba kwa kiasi fulani haukuwa wa lazima kutokea unaweza kusema viongozi wa wanaosimamia timu ya Taifa Stars walilazimisha matatizo wakati timu inajiandaa kwa safari ya Uganda na haukuwa na afya kwa matokeo chanya ya Taifa Stars. Nnaimani kabisa hata baadhi ya wachezaji walioambatana na timu hiyo kwa namna moja au nyengine lazima waliathirika kisaikolojia kwa kuwakosa wachezaji wenzao ambao wanafikiri uwepo wao ungeleta morali kwenye timu na kufanya kazi kuwa rahisi na baada ya wachezaji kukusanya nguvu zao nyingi za akili kufokasi na mchezo uliopo mbele yao nnaimani kabisa kuna wachezaji walitumia mda au siku kadhaa kuwaza kilichowatokea wenzao kitu ambacho hakikutakiwa kuwatokezea wachezeji hasa ukichukulia kipindi baina ya mechi hakikuwa na muda mrefu hapana shaka taharuki ile ilileta mazingira ya sumu katika bongo za wachezaji kisaikolojia. Wakati mwengine utaona hata timu ikiwa na mechi ya kirafiki basi huwaandilia mazingira rafiki wachezaji wake ili kuwaweka sawa kisaikolojia ni vitu ambavyo havihitaji hata kwenda shule hata timu za ndondo hawathubutu kuruhusu kitu kama hicho kitokee wapo tayari hata kumpapasa mtu na kiwembe tofauti zote baada ya mechi sio kabla mechi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pengo la nan labda uliloliona pale Leo. Or ndio ushabiki tu

      Delete
    2. Hamuishiwi maneno before match mlisema tutapigwa goal 8 eti kwa kuwa wachezaji Wa simba hawapo. Jamani tuachane na ushabiki tuisupport team tum support coach sio kutetea ujinga.

      Delete
    3. Binafsi, naamini mawazo ya Mwl tena yamesaidia saana timu kujituma.

      Aliwaeleza wazi wachezaji wote wanaocheza ligi ya nyumbani ,viwango vyao havipishani sana.

      Amekata kiburi.aungwe mkono. Sote tukemee ujinga kama vijana walivyojitoa kumuaminisha kocha hatotukuagusha.

      Delete
    4. Binafsi, naamini mawazo ya Mwl tena yamesaidia saana timu kujituma.

      Aliwaeleza wazi wachezaji wote wanaocheza ligi ya nyumbani ,viwango vyao havipishani sana.

      Amekata kiburi.aungwe mkono. Sote tukemee ujinga kama vijana walivyojitoa kumuaminisha kocha hatotukuagusha.

      Delete
  2. tuzd kuiombea timu yetu ya taifa isonge mbele

    ReplyDelete
  3. Uwepo wa john Boko kwenye mechi ile ungempa Mbwana Samata wasaa zaidi wa kufanya vitu vyake. Boko ni mshambuliaji wakati asilia akina Juuko na wenzake lazima wangekuwa kazi ya ziada tofauti na uzingizi waliokuwa nao jana katika mechi ile.

    ReplyDelete
  4. Ni kweli hata ile droo na lethoto kwakua wachezaji wa Simba hawakuwepo , unatakiwa ujue wachezaji wa Simba waviwango vya kawaida tu hata wasipokuwepo timu inapata matokeo

    ReplyDelete
  5. Ukiachilia mbali akina Samata wanaocheza nje kuna wachezaji kweli wanaopata changamoto ya kujitambua katika kazi yao kutokana na ushindani wa namba kama Simba? Labda Azam Afc lakini ndani ya miaka miwili mfululizo wachezaji wa Simba wamekuwa wakiandaliwa na kambi za maandalizi ya nje ya nchi chini ya makocha wa viwango vya juu barani Africa ambao wote walishabeba mataji makubwa Africa. Sidhani kama viongozi wetu wangekuwa ni watu makini na kazi yao wangelifanya ujinga wa kuwaacha wale wachezaji hata kama kwa kisingizio cha kusema kuwa kocha kasema waachwe. Kwani Amunike anauweledi gani juu ya wachezaji wa kitanzania?

    ReplyDelete
  6. Waganda washukuru Mungu kutimuliwa Bocco aliyewaliza Waganda jana na Kichuya mfagilia na mfungaji wa magoli na Kapombe mwenye pasi za macho ya miwani na yule aliyekuwa beki wa Azam

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic