September 20, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Maafisa wake, jana limetuma mpira wa mchezaji wa Stand United, Alex Kitenge baada ya kufunga mabao matatu 'Hat Trick' dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga na Stand United zilikutana Uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita ya Septemba 16 2018 na wenyeji kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3.

Katika mchezo huo Kitenge alifanikiwa kuifungia Stand mabao matatu na baada ya mechi hakupewa mpira baada ya kuelezwa kuwa TFF haina mipira ya kutosha.

Hatua hiyo liibua mjadala kwenye vyombo vya habari na mitandaoni na ndipo TFF walipojipanga kuanza mchakato wa kuutuma ili mchezaji huyo umeweze kumfikia.

Tayari imeelezwa kuwa uongozi wa Stand United umethibitisha kupokea mpira wa mchezaji wao ambaye alikuwa gumzo siku ya mchezo huo kwa kumlaza kipa wa Yanga, Klaus Kindoki na kusababisha kupokea lawama kuwa alifungwa kiulaini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic