September 20, 2018


Mwimbaji, Eddy Yawe, kaka wa Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) amekamatwa asubuhi ya leo na maofisa wa uwanja wa ndege wa Entebbe.

Mashuhuda wamesema Yawe alikataa kuandika taarifa ya polisi akisema alikuwa anamsubiri mwanasheria wake.  Haikufahamika ni kwa nini alitakiwa kuandika taarifa hiyo.

Bobi Wine alitegemewa kuwasili uwanja  wa kimataifa wa Entebbe saa nne asubuhi hii.

Wakati huohuo, polisi wameizingira nyumba ya mwanasiasa wa upinzani, Meya Erias Lukwago.

Pia,  nyumba ya mbunge wa Makindye Magharibi,  Allan Sewanyana, imezungukwa na polisi ambao hawajasema ni kwa nini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic