September 9, 2018


Na George Mganga

Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kinashuka Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wa kirafiki na African Lyon, kuna uwezekano mkubwa wa Nahodha wake, Kelvin Yondani kukosena.

Ukiachana na wachezaji Juma Abdul, Juma Mahadhi na Abdallah Shaibu walio majeruhi, Yondani naye ni anaweza akaukosa mchezo huo.

Yondani alishindwa kujumuika na kikosi cha Stars kilichoelekea Uganda kwa ajili ya kucheza mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Taifa hilo.

Kwa mujibu wa Daktari wa kikosi cha Stars, Richard Yomba, alisema beki huyo aliumia mguu hivyo ikabidi wambakize Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Yondani alikabidhiwa rasmi mikoba ya Unahodha Mkuu ndani ya Yanga baada ya aliyekuwa akivaa kitambaa hicho, Nadir Haroub Cannavaro kustaafu soka.

13 COMMENTS:

  1. Ongeleeni kuhusu ushindi mnono alioupata Simba Leo?Ndiyo mmesahau au mmeumia sana na matokeo!Saleh Jembe Fake news! Leo tunasubiri li bichwa LA habari lisemalo "Kikosi cha mauaji cha Yanga..Makambo ndani" Hamfai kabisa Saleh Jembe

    ReplyDelete
  2. George na wenzako mnaweza kufanya kazi nzuri zaidi ya hii mnayoifanya..hii blog haisomwi na upande mmoja pekee.tutawahama

    ReplyDelete
  3. Bin Zubery wameishasambaza habari ya Bocco..Nyie Subirini kuandika kwa kusifia Makambo leo.Hivi kweli hamkujua Simba wamepata goli nne.Saleh ni Fake news.Nahamia bin Zuberi

    ReplyDelete
  4. Wajomba acheni majungu,heri muombe ajira Salehe jembe anaweza waelewa. fitina na majungu ni kipimo cha akili ndogo ndo maana mkashabikia Uganda. Mnataka mambo yaende kwa namna akili zenu zinavotaka, its impossible.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti kwamba kuna watanzania Jana wameishangilia Uganda hiyo ni habari ya kizushi kama vile Saleh Jembe na Champion wanaavyoandika.Its unbelievable!

      Delete
    2. https://m.youtube.com/watch?v=H3PD4KqCUFs

      Ukweli ndiyo huo.were ni muongo kama hii blog ilivyo

      Delete
  5. Mxiojua mnajipongeza mmexhinda goli nyngi timu imejiokoteza wachezaji wake wngi wpo national team ya Kenya kweli nyie mbumbumbu mciojitambua mngecheza na kagera xugar au green warriors km kweli MNA team nzuri kuxikia wachezaji was leopard wapo timu ya taifa haraka haraka mkawaita mcheze friend match mpate kujixfia mmefunga goli nyngi muwasahaulixhe wanasimba ambao hawamtaki Hugo cocha was mieleka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini pia Kikosi cha Simba kilichoanza sio mile kinachoanza kawaida na wapo wachezi wanne Aishi , Okwi, Kagere na Chama ambao hawakuwepo sababu wanachezea timu zao za taifa. Saleh Jembe na Champion ni mabingwa wa kupika majungu.Fake New!

      Delete
    2. Hau hujui na wasimba wanne wako timu za mataifa yao

      Delete
  6. Saleh Jembe wanaandika habari utadhaji Uhuru inavyoandia au Tanzania Daima inavyoandika kuvutia kwake..Kama MTU anavuochagua gazeti basis ndivyo hivyo na sisi wasomaji tutachagua blog ya kusoma

    ReplyDelete
  7. Yaani hapa ni habari za Ulaya Simba na Yanga sana sana.Na za Simba na Yanga ni uzushi uongo na udaku unaoelemea upande mmoja.Jifunzeni kwa bin Zuberi huko kuna hata habari za mtibwa na Biashara.Saleh mnaweza Fanya kazi bora yenye ufanisi..Na mnajua hill acheni kujishusha hadhi!You are better than that!

    ReplyDelete
  8. Visingizio vyaanza mapema hofu ya kufungwa

    ReplyDelete
  9. Kwa maadili ya uandishi habari ikiandikwa anajitambulisha aliyeandika au hata blog au gazeti husema aliyeaandika ni mwandishi wao kutoka Dar,Mwanza ,Tanga n.k.Hii blog wanaojitambulisha ni George na Saleh...Habari nyingi zinachapishwa hata hatujui nani kaziandika..Hebu fuateni maadili ya kazi zenu!Acheni kuandika habari kihuni.Hatutaki vitu ambavyo sio professional.Havitufai!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic