October 1, 2018


Baada ya kuchezewa soka la maana na watani zao wa jadi katika Uwanja leo, mashabiki wa Yanga wameonekana kufurahia zaidi matokeo ya suluhu bila kufungana na Simba.

Simba na Yanga zilikutana jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara na mechi kumalizika kwa 0-0.

Katika kipute hicho Simba ilifanikiwa kutawala kwa kila kitu na kuwapa wakati mgumu Yanga ambao walicheza mfumo wa kujilinda zaidi na kushambulia kwa kuvizia.

Kutokana na hali hiyo, wapo baadhi ya mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiomba vema mpira ukaaisha haswa kuelekea mwishoni mwa kipindi cha pili.

Presha iliwapa wanayanga kutokana na pasi kibao ambazo Simba walikuwa wanaichezea Yanga nusu uwanja pamoja na mashambulizi makali kuelekea langoni kwao.

Pongezi zimfikie kipa wa Yanga, Beno Kakolanya ambaye aliokoka michomo mingi langoni kwake jambo ambalo liliwapa ugumu Simba kupata matokeo.

Katika mechi hiyo, Simba ilimiliki mpira kipindi cha pili kwa asilimia 38 huku Simba ikimiliki kwa asilimia 62.

2 COMMENTS:

  1. Mambo mazuri hayataki haraka. watanzania wengi ni watu wa viherehere. Nasema kwa kipindi kifupi alichokaa Simba kocha wa Simba Patrick Ausems amedhihirisha kuwa ni kocha wa viwango tena ni bonge la kocha. Simba inacheza mpira wa darasani kabisa na nnaimani suala la washambuliaji atalitafutia ufumbuzi muda si mrefu. Akipata muda zaidi ndani ya Simba huyu kocha atawaletea mapinduzi makubwa sana ya soka ndani ya klabu ya Simba.

    ReplyDelete
  2. yanga imecheza kama timu ndogo za Ndanda ambazo badala ya kucheza ili kupata ushindi zinapaki basi kulinda wana bahati washambuliaji wa simba hawakuwa makini vinginevyo wangepata bao moja tu yanga wangefungwa mengi maana wangefunguka na kutoa mwanya wa kufungwa zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic