October 24, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amelalamika juu ya ratiba ambayo wanaipitia kwa sasa ya kucheza mechi tatu ndani ya siku nane kwa kuwa haitoi muda wa kupumzika kwa wachezaji wake.

Aussems amesema kuwa ratiba kwao haijakaa sawa kwani inaweza kusababisha majeraha kwa wachezaji wake kwa kushindwa kutoa muda wa mapumziko baada ya kumaliza mechi moja.

"Kwa sasa tuna ratiba ngumu kidogo, kwani ndani ya muda mfupi tunacheza mechi tena, utaona tumecheza jumapili iliyopita, baada ya siku chache tunacheza tena na baada ya hapo tunacheza tena,kitu hicho ni kigumu kinaweza kusababisha matatizo kwa wachezaji," alisema.

Simba kuanzia Jumapili iliyopita hadi jumapili hii watakuwa na mechi tatu tofauti, walianza kupambana na Stand United wiki iliyopita, leo watacheza na Alliance na jumapili watacheza na Ruvu Shooting. 

1 COMMENTS:

  1. Sioni sababu ya Kocha kulalamika wakati ana Kikosi kipana na uwezo wa wachezaji wake hautofuatiani sana.Itakuwa vyema kama mechi ya leo akawatumia nusu ya wachezaji ambao muda mwingi wako benchi kama kina Dida,Bukoba,Mlipili,Salamba,Kwasi,Gyan,Dilungs,Rashid Mo ili kuwapa morali ya kuwa nao wanastahili kucheza mechi na hii italeta ushindani wa kupigania na pia itawapa wachezaji unafuu wa kupumzika kwa uwepo wa mzunguko wa wachezaji kucheza mechi.Kocha aache woga wa kuwatumia wachezaji wake wote waliosajiliwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic