October 1, 2018


Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema hana hofu kuhusu hatma yake ndani ya Old Trafford.

Mourinho anaamini kuwa maafisa wa klabu yake wamewasiliana na aliyekuwa kocha zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane.

Kocha huyo mwenye ambaye hapewi nafasi ya kuendelea kuinoa United kutokana na matokeo ya hivi karibuni kuwa mabaya, ameeleza maafisa hao wameanza mawasiliani ili waje wachukue nafasi yake.

Vyombo mbalimbali vya habari ulaya vimekuwa vikiripoti kuondoka kwa Mourinho siku za usoni jambo ambalo linapigiwa upatu na mashabiki wa timu hiyo.

Hata licha ya tetesi kuzidi kushika kasi, bado Kocha huyo ameendelea kuonesha imani ya kutokuwa na hofu yoyote ile haswa baada ya mechi iliyopita dhidi ya West ham kuchapwa mabao 3-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic