STARS YAINGIA KAMBINI KUWAWINDA CAPE VERDE
Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaanza rasmi leo kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Africa mwakani dhidi ya Cape Verde.
Kambi hiyo inayoanza leo itaanza na wachezaji wanaocheza ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.
Mazoezi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JKM Park,MNAZI Mmoja.
Maandalizi yatakuwa chini ya Kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi.
Madaktari Dr Richard Yomba na Gilbert Kigadya
Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12,2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment