October 24, 2018


Mambo ndani ya klabu ya Simba sasa yameanza kuwa vizuri baada ya mwekezaji wa timu hiyo Mohammed Dewji, 'Mo' kuwatumia ujumbe ambao umewashtua wachezaji wa Simba kutokana na uzito wake.

Hivi karibuni mambo ndani  ya klabu hiyo hayakuwa vizuri baada ya Mo kutekwa na watu wasiojulikana, viongozi na wachezaji walijikuta wakitumia muda mwingi kufikiria hatma ya kiongozi wao,ila baada ya kuonekana inasemekana ametuma ujumbe mzito ndani ya timu.

Kiungo mkabaji, Jonas Mkude amesema walikuwa na hofu baada ya kutekwa kwake, kwa kuwa ameonekana hofu hiyo haipo na nguvu imeongezeka baada ya kutuma ujumbe kupitia mmoja wa kiongozi wa Simba akiwataka kuendelea kupambana.

"Hofu haipo tena baada ya kupatikana kwa Mo na zaidi ametuma ujumbe kupitia kiongozi wetu akitutaka tuendelee kupambana uwanjani kwa ajili ya kutimiza malengo yetu yote tuliyokuwa tumejiwekea, salamu tumezipokea kwa mikono miwili na tutafanya mambo makubwa," alisema.

Simba imekuwa ikifanya vizuri kwenye michezo kadhaa ya hivi karibuni na kurejea kwa Mo ambaye hakuonekana kwa muda wa siku tisa kunaweza kusaidia kuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri, leo watacheza na timu ya Alliance Uwanja wa Taifa.

6 COMMENTS:

  1. Ila wachezaji wa Simba hasa washambuliaji wanatakiwa baada ya kumalizika kwa mechi wapitie mkanda wa video jinsi wanavyopoteza nafasi hovyo za wazi za kufunga ni makosa wanayoyarejea mechi baada ya mechi hata kichuya nae kawa si mtu makini tena wa kufunga magoli tatizo liko wapi? Ikiwa wachezaji wanatetemeka kutumbukiza magoli kwenye goli la stand united itakuwaje watakapokutana na Tp.Mazambe? Kwa jinsi wanavyocheza Simba kocha kamaliza kazi yake lakini inaonekana wachezaji hasa washambuliaji wanamuangusha kwani kwenye nafasi kumi za wazi timu inapata mabao mawili au matatu 3 is not enough,it is just wasting the hell of a good work. Kwa Simba ilivyo hata ikimpiga mtu goli saba nane mtungi sidhani kama timu husika watalalamika kwani Simba ni timu iliyokamailika. Najua wachezaji wenyewe pia wanaelewa makosa yao hivyo basi wanatakiwa kujirekebisha. Na kama wataendelea na tabia hiyo ya kukosa kosa mabao hovyo basi SIMBA wana kila sababu ya kufikiria kufanya usajili mwengine hasa kwa upande wa mshambuliaji makini alietulia na asiekuwa na hofu ya kutumbukiza mpira golini.

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli huu ujumbe unaosema "hofu haipo tena baada ya kupatikana kwa Mo na zaidi ametuma ujumbe kupitia kiongozi wetu akitutaka tuendelee kupambana uwanjani kwa ajili ya kutimiza malengo yetu yote tuliyokuwa tumejiwekea, salamu tumezipokea kwa mikono miwili na tutafanya mambo makubwa" NDIO ujumbe wa kushtua? Tuache kuwa tunachezeana akili kupitia vichwa vya habari ambavyo haviendani na habari iliyomo ndani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesema vema... wakati mwingine sielewi hata anataka kuleta ujumbe gani. Lichwa cha habari hakina uhusiano na anachoripoti!!!

      Delete
  3. kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza

    ReplyDelete
  4. Hii ni blog Moja ya havyo hapa Tanzania

    ReplyDelete
  5. daah huyu mwandishi wakat anaandika alikuwa na mawazo mengi maana haujui mwanzo wala mwisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic