December 14, 2018


Tottenham wameweka dau la kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Ureno Andre Gomes 26, ambaye anaichezea Everton kwa mkopo (Sun)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasemekana amekasirishwa na hatua ya bodi ya klabu hiyo kukaa kimya kuhusiana na masuala ya uhamisho. (Telegraph)

Manchester City wanapanga kuweka dau la euro milioni 50 kumnunua beki wa kushoto wa Leicester na England Chilwell, 21, mwezi Januari hasa ikizingatia kuwa Benjamin Mendy bado yuko nje ya kikosi baada ya kuumia. (Mirror)

Red Devils wanatarajiwa kuweka dao la kuvunja rekodi kumnunua beki wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly, 27.

Kuna tetesi kuwa Napoli wanataka takriban euro milioni 100 kumuachilia kiungo huyo wa kimataifa wa Senegal. (Evening Standard)

Mmiliki wa Newcastle, Mike Ashley anaamini kuwa mpango wa kuiuza klabu hiyo kwa kima cha euro milioni 300 utakamilika mwaka ujao. (Express)

Hata hivyo meneja wa Newcastle, Rafael Benitez amehakikishiwa kuwa atapewa fedha za kuwasajili wachezaji wampya mwezi Januari bila kujali kama klabu itauzwa au la. (Chronicle)

Meneja wa Leicester City, Claude Puel amegusia kuwa baadhi ya wachezaji watahama klabu hiyo mwezi Januari wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa. (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amethibitisha kuwa huenda akamsajili beki wa kati ifikapo mwezi Januari kwasababu kikosi chake cha ulinzi kimelemazwa kwa majeruhi. (Mail)

Kiungo wa kati wa Arsenal Emile Smith Rowe, 18, amekataa nafasi ya kusajiliwa na Barcelona na badala yake akaamua kusalia katika klabu yake ya utotoni. (Sky Sports)

Beki wa kushoto wa England, Danny Rose, 28, haoni haja ya Tottenham kuimarisha kikosi chao mwezi Januari. (Independent)

Real Madrid inatarajia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City Diaz, 19 kwa kima cha euro milioni 10 mwezi Januari mwakani. (ESPN)

Beki wa kushoto wa Uhispania Jordi Alba amesema mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 26, anakaribishwa kwa mikono miwili kujiunga Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkataba wa sasa wa Alba katika klabu hiyo unamalizika mwisho wa msimu huu. (AS)

Meneja wa PSV Eindhoven, Mark Bommel , amemuuliza mchezaji mwenza wa zamani Arjen Robben kuhusu uwezekano wake wa kuchezea ligi kuu ya Ujerumania.

Winga huyo wa mika 34 anajiandaa kuondoka Bayern Munich mwisho wa msimu huu. (Omroep Brabant - in Dutch)

Mshambuliaji wa Wolves wa miaka 27 Raul Jimenez, ambaye kwa sasa anachezea Benfica kwa mkopo, amesema hayuko tayari kuhamia Molineux kwa kima cha euro milioni 30 . (Mirror)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic