December 14, 2018




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba, Evans Aveva, Geofrey Nyange na Zacharia Hans Poppe licha ya upande wa serikali kuleta shahidi wa pili katika kesi hiyo, sababu kubwa ikielezwa kuwa ni kutokana mwendesha mashitaka kukabiliwa na majukumu mengine.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea jana Alhamisi baada ya mahakama kuomba upande wa serikali ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuleta shahidi wa pili katika kesi hiyo pamoja na yule wa awali ambao wote walifika mahakamani hapo.

Wakili wa serikali Leonard Swai alisema walileta mashahidi wawili katika kesi hiyo kama ilivyoamuliwa na mahakama huku shahidi wa pili akiwa ni mpya wakati huo shahidi wa kwanza ataendelea kumalizia ushahidi huo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye anasimamia kesi hiyo aliiomba mahakama kutoendelea na kesi hiyo  kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine ambayo ingechukua muda zaidi na tayari alikuwa ameanza kuisikiliza tangu juzi Jumatano na kesi hiyo isingeweza kusikilizwa kwa siku ya jana.

Baada ya kuahirishwa kesi hiyo inatarajiwa kuendelea  Desemba 19, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza ushahidi kwa upande wa serikali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic