December 29, 2018


Leo nawaletea Makocha wanne bora nchini kwa sasa

1. Patrick Aussems (Simba)

Kwa kuifikisha Simba hatua za Makundi hakuna shaka ni kocha mwenye uwezo mkubwa sana.

Mmoja wa wachezaji waandamizi wa Simba aliniambia hakuna kocha mwenye kujua mambo ya kiufundi kuliko 'Professor', katika makocha wote aliowahi kufundishwa na yeye,ingawa wakosoaji wa Aussems hawafurahishwi na kutumia washambuliaji watatu lakini kwa sehemu kubwa imelipa.

Sio maarufu sana kwa mashabiki labda kwa kuwa hana mbwembwe akiwa kwenye benchi ila wengi hawajui ni kocha anaependwa sana na wachezaji wa timu yake.

2. Mwinyi Zahera (Yanga)

Kimsingi ni kocha mzuri ukizingatia Yanga anaongoza Ligi kuu ingawa haivutii kisoka ila bado inashinda! Ana ushawishi sana kwa mashabiki wa klabu yake hata kama hujui falsafa wanayotumia Yanga uwanjani.

Wakosoaji wake wanadai anataka kuwa STAR kuliko wachezaji na ndiyo maana timu isipopata matokeo huwabebesha mzigo wao ila kiukweli ameisaidia Yanga ukizingatia hali yao kiuchumi kwa sasa!! Naarifiwa si maarufu kwa wachezaji wengi kikosini.

3. Hans Van Plujium (Azam FC)

Ana maarifa sana katika eneo la kimbinu na anaijua vema TPL, amethibitisha pasi na shaka ni kocha professional! Ingawa hatujaiona Azam ikicheza soka maridhawa ila inafanya vema na pia ameweza kuwapa muda wa kucheza wachezaji ambao walishaanza kusahaulika kama kina Singano.

Binafsi ninapoenda mpirani katika mechi zisizohusu timu yake hupenda kukaa naye sababu ni mchambuzi mahiri wa soka na kuna mengi anayo kuhusu kandanda.

Wakosoaji wake hudai anakariri sana mambo na ni vigumu kubadilika badilika kimbinu na kiufundi.

4. Zuberi katwila (Mtibwa Sugar FC)

Nimemfahamu kocha huyu kijana miaka mingi, tukianzia kucheza pamoja mm na yeye katika klabu yetu iliyokuwa maarufu Kariakoo, Mafia Mob, akicheza ndani kushoto na mimi nikicheza kulia na kuipandisha hadi daraja la tatu zama hizo.

Ni mtu wa soka na ana weledi wa kikocha ukizingatia hapendi sifa sifa kama baadhi ya makocha walivyo.

Anajua sana kuvumbua wachezaji na akipata fursa kubwa, mengi tutayashuhudia kwake kama nchi.

Wakosoaji wake hudai hupenda sana kuwapanafasi wasaidizi wake kiasi cha kutobaki na misimamo yake kama kocha mkuu.

Na Haji Manara (Ofisa Habari wa Simba)

6 COMMENTS:

  1. Kwaiyo, kiuchambuz wa manara. Kama ungetoka chambuz wako kabla ya club bingwa, ipi nafasi halis ya aussem(kocha wa simba) hapo.

    ReplyDelete
    Replies

    1. Bila Club bingwa simba pia isingekuwa na viporo, kwa angebaki kuwa wa kwanza tu

      Delete
    2. hapa ndio umeongea nini wewe ?unge unge ndio nini jambo lishakuwa sasa achana na hizo unge,na mimi nikuulize JE, YANGA INGEKUWA HAIONGOZI LIGI NAFASI YA ZAHERA INGEKUWA IPI?

      Delete
  2. Kwa zahera huyo patrick Aussems ataxubili
    Anapata kila kitu lkn kikos chake na mbinu zake hana jipya
    Kocha bora in zahera na pluijim ndio wanaostahili kuwa namba moja na namba mbili ambao tayari wametwa hadi tuzo ya kocha bora wa mwezi

    ReplyDelete
  3. Ameangalia kochawa timu inayocheza kimataifa ingawa Mimi ni mshabiki wasimba mwinyi zahela ni borakuliko patrick

    ReplyDelete
  4. unaipenda simba mpaka huzijui timu nyingine zinachezaje?simba inawachezaji wenye vipaji ila haina kocha bora mfano goli la tatu la simba vs nkana ni la mfumo au juhudi binafsi za wachezaji?maana mfumo ulikufa ikabakia tusubiri tuone ndio goli likatokea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic