December 30, 2018

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Coastal Union, Ally Kiba ambaye anafunga mwaka akiwa na bao moja alilofunga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market ya Morogoro amekuwa chachu ya mafanikio kwa wachezaji.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema amekuwa akiwapa moyo wachezaji wenzake hata asipokuwa na timu hali inayofanya kila mchezaji kuthamini uwepo wake ndani ya kikosi.

"Ni mchezaji ambaye hana makuu akiwa na timu, mwepesi kuelewa na kuelekeza wenzake pale anapoona wamekata tamaa ya kutafuta ushindi, ana mambo mengi ambayo anayafanya ila haachi kuwa nasi kwa kuwa tumemsajili ili aitumike timu na hicho ndicho anachokifanya," alisema.

Coastal Union wanafunga mwaka wakiwa nafasi ya 7 kwenye ligi baada ya kucheza michezo 16 na kufanikiwa kujikusanyia pointi 24 huku Kiba akiwa amecheza dakika 64 za nguvu mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic