December 11, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa bado wachezaji wake wanapaswa kuendelea kupambana katika michezo yao ya Ligi Kuu ili kupata matokeo chanya.

Zahera amesema kikubwa ambacho kinamfanya aweze kupata matokeo ni uwezo wa wachezaji wake kukubali kuonyesha juhudi binafsi wakiwa uwanjani pamoja na nidhamu ya kufuata maelekezo.

"Hakuna mchezo mgumu na mwepesi kwenye ligi ambao unanifanya nihofie, wachezaji wangu wana tambua majukumu yao na kufanya kazi kwa ushirikiano, ugumu upo ila nina waambia wachezaji wacheze kama wamefungwa ili kupata matokeo," alisema.

Yanga imefanikiwa kucheza michezo 15 na wamepata sare 2 tu katika michezo hiyo wakiwa ni vinara wa ligi kwa kujikusanyia pointi 41.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic