Timu ya Yanga imeweka usawa baada ya kusawazisha bao la Mangalo katika mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Biashara United na kufanya mabao kuwa 1-1 katika mchezo unaochezwa uwanja wa Taifa leo.
Biashara United walianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Abdulmajid Mangalo dakika ya 37 akiwa nje ya 18 kwa kuachia shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango Ramadhani Kabwili.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amefanya mabadiliko kwa kumtoa Rafael Daud dakika ya 41 nafasi yake ikachukuliwa na Papy Tshishimbi.
Kasi ya mpira kwa timu zote uwanjani ni kubwa huku Yanga wakikosa nafasi za wazi kwa washambuliaji wake walio chini ya mkongomani Herieter Makambo.
Kipindi cha pili kimeanza Amiss Tambwe anaingia dakika ya 53 kuchukua nafasi ya Thaban Kamusoko, pia Salum Abdalah' Fei Toto' alitoka dakika ya 67 akaingia Pius Buswita.
Abdalah Shaibu 'Ninja' anmaandika bao la kwanza akiwa ndani ya 18 na kuweza kuweka usawa kwa timu zote mbili na Herieter Makambo anafunga bao la ushindi dakika ya 80.
0 COMMENTS:
Post a Comment