December 19, 2018




Mshambuliaji wa timu ya KMC, James Msuva ameonyesha kwamba yeye si mchezaji wa mchezomchezo  akiwa ndani ya eneo la hatari baada ya kufanikiwa kuwafunga Simba bao la kufutia machozi dakika ya 68.

Bao hilo ambalo linamfanya Msuva afikishe mabao 5 kwenye Ligi amelifunga baada ya mlinda mlango wa Simba, Deogratius Munish 'Dida' kutema shuti matata lililopigwa na Elias Maguli likawa linaambaa kwenye 18 akakutana nalo na kuachia shuti kwa mguu wake wa kushoto.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni kiporo, Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambayo yote yalifungwa kipindi cha kwanza na Adam Salamba dakika ya 12 na Said Ndemla dakika ya 14.

Simba wanafikisha pointi 30 wakiwa wamecheza michezo 13 wakiachwa kwa jumla ya pointi 14 na Yanga ambao kesho wanacheza na African Lyon katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kutokana na ombi maalumu la Lyon.

5 COMMENTS:

  1. Kikosi ambacho huwa wanaingia kama substitute kimeondoka na point tatu toka kwenye timu iliyoitoa jasho Yanga.This is Simba wengine wako kwenye safari tu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna mijitu ni pumba toka asubuhi,kwani hao akina Kichuya sio wachezaji wa Simba?Naona umeshalewa na harufu ya xmass bora ukatafute Noah kule kwenu Kimesera!
      Yanga ilishinda bila ya kufungwa na hao KMC wakati nyie mikia metobolewa na hao,sasa nani Zaidi?

      Delete
    2. Hasira za nini Babu, HII NDIO SIMBA.

      Delete
    3. mahasla ya nini....dhis iz thimba

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic