December 19, 2018



Kikosi cha Simba kinaongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo unaoendelea kuchezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo ambapo dakika 90 zimekamilika.


Mabao ya Simba yamefungwa na Adam Salamba dakika ya 12 akimalizia pasi ya Haruna Niyonzima na Said Ndemla akifunga bao la pili dakika ya 14.

Bao la KMC limefungwa na James Msuva ambaye alitumia vema makosa ya mabeki wa Simba kwa kuachia shuti kali lilomshinda Dida.

Kila timu imepambana kutafuta matokeo, huku mchezaji wa Simba beki anayepanda na kushuka akionyesha juhudi za kutafuta mpira uwanjani na Elias Maguli wa KMC akitafuta mbinu za kumtungua mlinda mlango  wa Simba.

4 COMMENTS:

  1. Duuh Kikosi kipana kinafanya yake kila la kheri chama langu...wengine tupo safarini lol

    ReplyDelete
  2. Ningefurahi sana kama kocha Simba atawapa nafasi Rashid Juma, Dilunga na Ndemla kucheza na Nkana pia Asante Kwasi, Salama na Coudibary. Kikosi cha Simba kweli kipana

    ReplyDelete
  3. Zahera ameaibikaje..Alikuwa anauliza kwa Simba INA viporo..Sasa wamekimaliza kiporo vizuri kwa kutumia kikosi mbadala..Na kuipanga Simba kucheza ligi Leo halafu baada ya Siku NNE wacheze na Nkana sio jambo jema.Aussens ana akili sana...ni kocha mzuri

    ReplyDelete
  4. Ila mwandishi duuuuh!!!!!!! habari in para 4, kama vile haukuwepo uwanjani? Mbona za wengine unatoa kwa urefu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic