December 30, 2018


Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anakuna kichwa kumwanzisha Marcus Rashford au Anthony Martial kama straika wa kati kwenye kikosi chake wakati timu  yake itakapoikabili Bournemouth leo Jumapili kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Solskjaer amekuwa anampanga Rashford kama straika pekee kwenye mechi zake mbili ambazo amekuwa
akiinoa timu hiyo wakati ilipoicharaza Cardiff mabao 5-1 na ilipopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Huddersfield.

Katika mabao hayo nane kwenye mechi mbili, Rashford amefunga bao moja kwa `free kick’ kwenye mechi dhidi ya Cardiff City.

Pamoja na Rashford kutofunga mabao mengi lakini ameonyesha kiwango kikubwa kutokana na kujituma uwanjani. Rashford anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Martial, ambaye katika siku za karibuni amekuwa mzuri katika kupachika mabao.

Martial ametokea kuwa tegemeo la Manchester United akiwa ametupia mabao tisa katika mashindano yote msimu huu

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic