December 29, 2018


Kiungo aliyesajiliwa kwa mbwembwe nyingi ndani ya kikosi cha Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi Kabamba, amedaiwa kuwazimia simu viongozi wa timu hiyo tangu walipompatia ruhusa ya kwenda kwao DR Congo kwenye matatizo ya kifamilia jambo ambalo limezua taharuki klabuni hapo.

Takriban wiki tatu zilizopita, Tshishimbi aliuaga uongozi wake kuwa amefiwa na mama mkwe wake, hivyo akaomba ruhusa ya siku saba ili akaione familia hiyo lakini tangu alipoondoka sasa ana zaidi ya wiki tatu hapatikani hewani na wala hajasema kinachomfanya asirejee kwenye majukumu yake.

Kikizungumza na Championi Ijumaa chanzo cha ndani ya Yanga kilisema nyota huyo amekuwa na tabia ya kuigomea Yanga akishinikiza malipo ya mishahara yake mara kwa mara, hivyo inawezekana wazi alipopata safari ya kwenda kwao umekuwa ni muda muafaka kwake kuwazimia simu kushinikiza malipo hayo.

“Kweli tangu Tshishimbi alipoaga kwenda kwao ana zaidi ya wiki tatu sasa hatumpati tena hewani wala hajawasiliana na uongozi kusema chochote jambo ambalo hata sisi linatutatiza, ila tunaamini atakuwa ameamua kujipumzisha tu kwani kabla hajaenda kwao alitoka kwenye majeraha ya muda mrefu kiasi kwamba alihitaji kupata muda wa kupumzika.

“Tunategemea kama atakuwa hajapata tatizo lingine basi siku chache zijazo atarejea na kuungana na wenzake ingawa naye ni binadamu, yawezekana kweli kuna kitu aidha nje au ndani ya kazi kinachomtatiza kiasi cha kumfanya ashindwe kuwasiliana nasi kwani ni wazi alisafiri kwenda kwenye matatizo ya kifamilia,” kilisema chanzo.

CHANZO: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. Dah wabongo na habari zisizo na uhakika bwana washakula mb za bando langu bureee aaggghhffghhh

    ReplyDelete
  2. Mtu mwenyewe kachuja cku hz mwache aendelee kujimaliza coZ hata akicheza cku hiz anarukaruka tu c Tshishimbi yule wa moto

    ReplyDelete
  3. Jamani viongozi wayanga tafuteni hela muwalipe wachezaji mishahara yao mbona wachezaji wanajituma Sana uwanjani na wanapata matokeo mazuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic