December 9, 2018


Tazama wakati mbwa koko alipookoa bao katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini Argentina, mechi kati ya Defensores de Belgrano de Villa Ramallo na Juventud Unida de GualeguaychĂș.

Belgrano walishindwa 3-0, lakini bila msaada wa mbwa huyo, huenda wangefungwa mabao zaidi.

Bao lililozuiwa na mbwa huyo halikuhesabiwa.

Katika mechi hiyo ya Jumapili iliyochezewa uwanja wa klabu ya Juventud Unida de GualeguaychĂș mwendo wa saa tatu hivi kwa gari kaskazini mwa Buenos Aires, klabu hiyo ilikuwa imewadhibiti vyema washambuliaji wa Defensores pale kipa wa Belgrano Brian Leandro Olivera alipofanya kosa kubwa eneo la hatari.

Aliuchukua mpira na akidhani kwamba anaupiga kuelekea eneo salama katikati mwa uwanja ukamgonga mchezaji wa Juventud na kuanguka miguuni mwa adui huyo.

Hakusita, bali alipiga shuti kali kuelekea kwenye goli lililokuwa wazi, bila mlinzi.

Lakini mbwa koko huyo, katika pita pita zake akawa anapitia mbele ya lango na kuuzuia mpira huyo, kisha akatimua mbio na kwenda zake.

Sheria za FIFA husema klabu inafaa kuwachezesha wachezaji 11 uwanjani pekee wakati mmoja.

Lakini mbwa ni mchezaji? Kwa wengine amekuwa shujaa, lakini kwa wengine mhuni.

Kisa cha mbwa huyo kimetumiwa na mengi kama kiashiria cha tatizo la mbwa wa kurandaranda. Hatua zimekuwa zikichukuliwa zikiwemo kuwakamata mbwa koko na kuwaua wale wakongwe.

Inakadiriwa kwamba asilimia 78 ya kaya nchini Argentina humiliki mbwa, kiwango ambacho ni cha juu kuliko mataifa mengine ya Amerika Kusini.


Kwa mujibu wa BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic