January 10, 2019


Kiungo mwenye vionjo vya kipekee ndani ya kikosi cha Simba, Claytous Chama raia wa Zambia ameweka wazi kwamba ndani ya kikosi cha Yanga kuna wachezaji watatu anaowazimia akiwemo Ibrahim Ajibu.

Chama ambaye amekuwa na msaada mkubwa ndani ya Simba, amekuwa akifananishwa

na Ajibu kutokana na aina yao ya uchezaji uwanjani huku wote wakiwa na vikorombwezo vingi.

Kiungo huyo wa zamani wa Power Dynamos ya Zambia, ametamka wazi kuwa ndani ya Yanga anawakubali Ajibu, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Kelvin Yondani.

Chama mwenye miaka 27, amesema kwamba anakoshwa na Ajibu ndani ya kikosi hicho cha Yanga kinachonolewa na Mkongo, Mwinyi Zahera.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa ana mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, amefafanua kwa kusema: “Wachezaji ambao ninawazimikia pale Yanga ni Ibrahim Ajibu, Fei Toto sambamba na Yondani.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic