October 14, 2021


 KUNA namba za jezi ambazo huwa zinastaafishwa na kuwekwa kabatini mazima huko majuu Kibongobongo huwa inakuja kisha inakataa lakini leo acha tucheki zile za mbele kwanza namba za jezi ambazo zilistaafishwa kutokana na sababu mbalimbali.


Kwa timu ya Birmingham City jezi namba 22 iliwekwa kabatini na hakuna mchezaji ambaye atakuja kuitupia tena na sababu ya jezi hiyo kustaafishwa ni baada ya Birmingham kuwapa heshima ya kuvunja rekodi ya uhamisho klabuni hapo wakimuuza kiungo wao Jude Bellingham kwenda Klabu ya Borussia Dortmund kwa pauni milioni 25.


Namba 10

2000 Klabu ya Napoli walikubali kuistaafisha jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na legend, Diego Maradona na hiyo ilikuwa ni kutokana na mchango wa nyota huyo aliyedumu miaka 7 katika timu hiyo.

Aliweza kutimiza majukumu kwa timu yake kutwaa taji la Serie A mara mbili ambayo wanayo mpaka sasa.

Timu ya taifa ya Argentina ilitaka kufanya hivyo mwaka 2020 ila Shirikisho la Soka la Kimataifa, (Fifa) liliweka ngumu. Kwa sasa nyota huyo ametangulia mbele za haki.


Namba 6

West Ham United ukienda pale hata kama unaufundi kiasi gani namba 6 sahau huwezi kupata kwa sababu ilistaafishwa kwa ajili ya heshima ya beki wa timu hiyo na nahodha Bobby Moore.

West Ham walifanya hivyo mwaka 2008 na tangu wakati huo hakuna ambaye amepewa jezi hiyo pia kuna sanamu ya nyota huyo nje ya uwanja wao wa London.

3 na 6

AC Milan 2009 mwaka ambao Paolo Maldin aliichezea AC Milan msimu wake wa mwisho mabosi wa timu hiyo nao wakachukua maamuzi kuipumzisha jezi no 3 ambayo ilikuwa inavaliwa na mkongwe huyo.


Aliweza kushinda taji la Seria A mara 7, alisepa na mataji matano ya Ulaya na alitumia maisha yake ya soka ndani ya timu hiyo na jezi hiyo atapewa moja ya watoto wa Maldin pale atakapoichezea timu ya wakubwa.

Pia AC Milan imeiweka kando namba 6 kumpa heshima kiungo wao Franco Baresi ambaye anakumbukwa kuichezea timu hiyo kwa miaka 20.


Namba 14

Alipotimiza miaka 60 mwaka 2007, Johan Cruyff klabu yake ya Ajax ilitangaza kutoitumia jezi namba 14 iliyokuwa inavaliwa na mwamba huyo aliyetwaa tuzo ya Ballon d'Or mara tatu .

Manchester City namba 23

2003 dunia iliingia kwenye simanzi kutokana na tukio la kuanguka kisha kufariki kwa kiungo wa Cameroon,  Marc-Vivien Foe katikati ya uwanja wakati akiitumikia timu yake ya Cameroon. 

Wakati huo Foe alikuwa akiichezea City kwa mkopo akitokea Lyon ya Ufaransa kutokana na tukio hilo Manchester City waliamua kutoitumia jezi hiyo namba 24 kwa ajili ya kumpa heshima. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic