July 21, 2021

KLABU ya Azam inaendelea kuonyesha makucha yake katika dirisha la usajili wa wachezaji wapya ambapo leo wamemtangaza rasmi, Kenneth Muguna na kufanya idadi ya nyota wapya waliosajiliwa na klabu hiyo mpaka sasa kufikia wanne.

Huu hapa usajili wa Azam mpaka sasa;

Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Charles Zulu, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Cape Town City ya Afrika Kusini.

 

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco ya huko.

 

Beki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama, kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting


Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya huko.

8 COMMENTS:

  1. Katika usajili wote niwe mkweli kabisa kwa Muguna Azam wamekera Sana huyu jamaa anajua binafsi nilitamani klabu yangu pendwa ya simba kumsajili huyu mwamba lakini wakati mwingi viongozi wetu wa simba huwa wagumu kufuatilia Maoni ya wadau na huwa hawamuoni mchezaji mpaka wasikie timu fulani inamfuatilia mchezaji huo au amesajiliwa na timu fulani. Kama alivyokuwa Onyango Muguna ni jembe hasa pengine kuliko Onyango binafsi nilitarajia simba wangemsajili Kenneth Muguna kwanza kabla ya Onyango.Tunajua ndani ya Simba tayari tuna idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni ila partnaship Kati ya mchezaji na mchezaji uwanjani siku zote ni Jambo muhimu na partnaship ya Muguna na Onyango ndio inayotengeneza uti wa mgongo wa timu ya Taifa ya Kenya kwa muda Sasa. Kwa hapa Azam wameramba dume ila niwakumbushe Tena timu yangu pendwa ya simba kuwa Bwana Mdogo Phiri wa Zambia ni zaidi ya Louis Miqisone na wamekuwa na tetesi nae ila nahofia Azam wanaweza kumtangaza wakati wowote kuanzia Sasa.

    ReplyDelete
  2. Simba wana mawakala ambao hawana papara Muguna ni mchezaji wa kawaida sana kwenye timu ya simba. Simba inataka cream ya wachezaji una Bwalya una Aucho una Lwanga una chama una Luis una Mugalu juu una striker mpya (Uknown) + Watu wapya Muguna Gormahia wamemuacha kwa sababu wamemuona msaada wake ni mdogo. Azam bado anajenga timu yake Lwandamina kafanya kama Kaze kwa kina fiston na saidoo. Atawajaza wengi tu Zanaco Imeshuka kiwango Gormahia ndio usiseme kama ihefu vile....... Muda utaongea kikubwa tuwapongeze Azam ila bado wanahitaji changes kubwa sana

    ReplyDelete
  3. Kwa Muguna time will tell Kama ni wa kawaida au la? Mpira ni mchezo wa wazi.

    ReplyDelete
  4. Tuacheni unafiki bwana huyu bwana mdogo ni mzuri Gor Mahia si kwamba wamemwacha aligoma kusaini mkataba mpya na kwa sasa gor Mahia wameyumba kidogo kiuchumi wasingemwacha kwa gharama yoyote ile

    ReplyDelete
  5. AZAM FC ovyo tu aiseee yani usishangae msimu ujao wakashika nafasi ya 5

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mhhhhh watakupiga ja wewe una ona kwasababu wamekukazia ligi kuuu Ndio useme wako ovyo next watakupigaaaaa

      Delete
  6. Duh! Uovyo wa Azam uko wapi jamani! Toa sababu za hukumu yako.

    ReplyDelete
  7. Kama wamesajili vizuri tuwape pongezi zao ili watuwakilishe vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na walitangaze vyema soka la Tanzania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic