January 17, 2019


Yanga imezidi kuneemeka na michango ya mashabiki baada ya kupokea zaidi ya shilingi 700,000 za kitanzania juzi ilipocheza dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga iliibuka kinara kwa ushindi wa mabao 3-1, baadhi ya mashabiki wa Yanga walikuwa wanachangisha fedha ndani ya uwanja.

Mashabiki hao walijitoa kwa hali na mali na kuacha kufuatilia mpira badala yake wakawa wanakusanya fedha na kufanikiwa kufikisha kiasi hicho.

Ikumbukwe si mara ya kwanza kwa wanayanga kuchangisha fedha hizo uwanjani bali imekuwa ni kama jambo la kawaida hivi sasa.

Michango hayo imekuwa ikishika kasi kutokana na klabu kuyumba kifedha tangu kuachia ngazi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu, Yusuf Manji.

2 COMMENTS:

  1. Laki 7 ni neema! Givet me a break. Huwezi hata kulipia malazi ya siku moja kwa wachezaji.
    Wakati mwingine andikeni uhalisia .

    ReplyDelete
  2. Wazitafute kwa jasho , walishindwa kupeleka kikosi cha ushindani kombe la mapinduzi wangepata 10 au 15 . wazembee na sports pesa wajanja wanyakue mshiko wao wakalie ombaomba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic