February 1, 2019


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumsajili Mshambuliaji Vitalis Mayanga, kutoka Ndanda FC ya Mtwara.

Usajili huo unaelezwa ni kutokana na matakwa ya Kocha Mkuu wa timu, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Baada ya kukamilisha usajili wake, uongozi umesema tayari umeshafanikisha kupata leseni yake maalumu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayoendelea hivi sasa.

Mbali na Mayanga, Simba wamesema vilevile wamepata leseni ya Mburkinafaso, Zana Coulibaly ambaye alikuwa hajapata bado.


Kikosi cha Simba kesho kitakuwa kinashuka dimbani kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahlu huko jijini Alexandria, Misri ukiwa ni mchezo wa kundi D.

1 COMMENTS:

  1. Wakija Simba moto tao unapoa kabisa hawachezi kama walikotoka. Salamba katuangusha sana Simba. Ngoja tuone huyu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic