February 20, 2019



MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo ameonyesha ufundi wake leo baada ya kuanza kuzamisha jahazi la Mbao FC kwenye mchezo wao wa leo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya Amiss Tambwe kumaliza kazi.

Mbao walianza kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa Ndaki Robert na kuifanya Yanga isubiri mpaka kipindi cha pili kusawazisha kupitia kwa Heritier Makambo dakika ya 49.

Dakika ya 67 Eric Mulilo wa Mbao alinawa mpira eneo la hatari na kufanya mwamuzi atoe penalti iliyowekwa kimiani na Tambwe dakika ya 68.

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 61 ikiwa kwenye  namba moja kwenye msimamo na kuiacha Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 42.

Simba ina michezo nane mkononi inaachwa kwa jumla ya pointi 19 na pia Azam FC wenye pointi 50 wakiwa wamecheza michezo 24 wameachwa kwa jumla ya pointi 11 na Yanga.

5 COMMENTS:

  1. Hujielewi kijana yanga hawezi mpoteza simba hata kidogo angalia ubao ndio utakupa tathmin,bingwa simba angalia mechi alizocheza alama alizonazo na magoli ya kufunga nakufungwa ndio utajua nani bingwa mpaka sasa kipa bora ni aishi manula,kwanza kafungwa magoli machache na amekusanya clean sheet kibao,vyura jipangeni sana bado.

    ReplyDelete
  2. Hujielewi kijana yanga hawezi mpoteza simba hata kidogo angalia ubao ndio utakupa tathmin,bingwa simba angalia mechi alizocheza alama alizonazo na magoli ya kufunga nakufungwa ndio utajua nani bingwa mpaka sasa kipa bora ni aishi manula,kwanza kafungwa magoli machache na amekusanya clean sheet kibao,vyura jipangeni sana bado.

    ReplyDelete
  3. Mwandishi naona bado una maluweluwe ya kufungwa na Simba.Sasa anampotezeaje Simba?

    ReplyDelete
  4. Kuleni kwanza hivo viporo vyenu vyote mkumbane na ladha yake ndo muanze kumsakama mwandishi,'Daima mbele nyuma mwiko'

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic