KAGERE ATUMA UJUMBE KWA MABOSI WAKE SIMBA
Straika Mrwanda, Meddie Kagere anayekipiga katika klabu ya Simba, amesema shangwe na upendo anaoupata hapa Tanzania haijawahi kutokea popote pale kwenye maisha yake ya soka.
Kagere ameamua kuweka wazi suala hilo kutokana na mwitikio wa wanachama na mashabiki wa Simba namna wanavyompa hamasa ya hali ya juu akiwa dimbani.
Ameeleza kufarijika zaidi kuwepo ndani ya timu ya Simba tofauti na wakati akiichezea Gor Mahia FC ya Kenya kwa kusema hakuwahi kupata ile furaha ambayo anaipata akiwa na Simba hivi sasa.
Kagere ambaye amesaidia Simba kupata mabao muhimu katika mechi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly na Ligi Kuu dhidi ya Yanga amewataja pia mabosi wake kwa mchango wanautoa kwa wachezaji wote.
Amemwaga pongezi zake akieleza wanapatiwa kila kitu ikiwemo mishahara yao tena kwa wakati jambo ambalo timu nyingi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zinashindwa kutekeleza.
"Nafurahia sana maisha nikiwa ndani ya Simba kwakuwa ni ya kitofauti na wakati ule nikiwa Gor Mahia ya Kenya, pongezi ziwafikie uongozi wetu kwa kututimizia mahitaji muhimu ikiwemo mishahara tena kwa wakati" alisema.A








Simba Taifa kubwa na mwenye kujitahidi basi hakosi kufanikiwa. Jambo moja kubwa kwa wachezaji wa Simba na kagere awe kiongozi wanatakiwa kucheza mechi moja muhimu ya jihadi itakayowajengea heshima ya kihistoria katika maisha yao ya soka na mechi hiyo ni mechi zidi ya Js Saoura ugenini Algeria. Kama ni somo la vipi wachezaji wa Simba wamejifunza jinsi ya kucheza ugenini basi mechi mbili kati ya As vita na Alahly zinatosha kabisa kuwapa somo la jinsi gani ya kwenda kupata matokeo tofauti nchini Algeria zidi ya yale mabaya waliyoyapata kule Congo na Misri kwani simba mechi yao zidi ya Js Saoura naweza kusema ni kama fainali kwao ni mechi ya kuwapeleka robo fainali club bingwa Africa.
ReplyDeleteKagere ni muungwana na mkweli. Mazuri anayotendewa anayapokea kwa mikono miwili na hasiti kulipa fadhili. Jambo hilo ni muhimu sana kwani ni funzo kwa wote waliobakia na kutokana na hayo ndipo alipokuwa kipeenzi hata kwa baadhi ya wachezaji wanaoitakia mabaya Somba. Hapana kitu kizuri kuliko kupendwa na hana ubaya au chuki za kijinga kwa yeyote
ReplyDelete