February 24, 2019


STAA wa Yanga Mkongomani, Heritier Makambo amefurah ishwa na kiwango kikubwa cha hivi sasa ambacho amekionyesha kiungo wa timu hiyo, Papy Tshishimbi.

Kauli hiyo, aliitoa mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara na Mbao FC uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 huku Makambo akifunga bao kwa kichwa akitumia krosi safi ya Tshishimbi.

Tshishimbi ameonekana kurejea kwa kasi kubwa akitokea kwenye majeraha ya goti aliyoyapata kwenye michezo ya mwanzo ya ligi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Makambo alisema kiungo huyo ni kati ya wachezaji anaopenda kucheza nao pamoja katika timu hiyo kutokana na kiwango kikubwa alichokuwa nacho. Pia kiungo huyo anacheza kwa kufuata maelekezo ya kocha huku akitimiza majukumu yake ya kuchezesha timu na kukaba ndani ya wakati mmoja.

“Kwanza nimshukuru Tshishimbi kwa pasi nzuri aliyonipa katika mchezo uliopita wa ligi tulipocheza na Mbao, kiukweli anastahili pongezi kutokana na jitihada kubwa aliyoifanya katika kupiga krosi kabla ya mimi kufunga kwa kichwa.

“Kiukweli kutokana na ugumu wa ile mechi, Tshishimbi alijitahidi kufanya kazi yake vizuri ya kuchezesha timu kwa maana ya kupiga krosi na pasi safi na kukaba ndani ya wakati mmoja.

“Hivyo, nimpongeze kwa hilo Tshishimbi akiwa ametokea kwenye majeraha, ni matarajio yangu kumuona Tshishimbi akiendelea kuongeza kiwango chake katika michezo ijayo ya ligi na Kombe la FA,” alisema Makambo.

2 COMMENTS:

  1. Mzee mbona maludia ludia matukio si mpige kimya kama hamna jipya mnashusha hadhi ya blog

    ReplyDelete
  2. Wanamsifu mfululizo ili alainike asije kuwakimbia kwani zimeshakuwa zinapigana kikumbo kwakumtangulizia dau nono zipate saini yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic