February 23, 2019



Wanachama wanne wa Yanga maarufu kama "Makomandoo" wamefikishwa polisi baada ya vurugu kuibuka.

Makomandoo hao kutokea Lindi mjini wanatuhumiwa kumfanyia vurugu meneja wa uwanja wa Namungo mjini Namungo.

"Unajua wale wametokea Lindi Mjini, sasa walitaka kila aliye uwanjani atoke. Maneja akakataa kwa kuwa waliokuwepo walikuwa mafundi katika ujenzi. Kukataa kwake kukawaudhi hao makomandoo ambao wakaanza mzozo na kufikia kumsukuma," kilieleza chanzo.

Makomandoo hao walichukuliwa na askari kwa mahojiano na haijaelezwa kama tayari waliachiwa kwa dhamana au la.

Yanga ipo mjini humo kuwavaa wenyeji wake Namungo FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho, kesho.


4 COMMENTS:

  1. Mafundi ujenzi wanajenga nini siku moja kabla ya mechi? Mnajitakia fujo nyingine nyinyi mameneja wa viwanja

    ReplyDelete
  2. Kwani uliambiwa wanajenga sehemu ya kuchezea mpaka uhoji wanajenga nini siku moja kabla ya mechi acha ushabiki usiokua na maana

    ReplyDelete
  3. Kwani hao wanaotaka wabaki peke yao ili iwe nini? Ushirikina hausadii chochote kwenye mpira.
    Kama mafundi walikuwa wana kazi ya kufanya wewe nani uhoji kuwepo kwao???

    ReplyDelete
  4. Nyie mashabiki wa Mikia mtapata taabu sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic